Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepokea msaada wa Makopo 134 ya Rangi za Coral Paint kutoka kampuni ya Insignia Ltd kwaajili ya Kupendezesha Mandahari ya Jiji la Dar es salaam.
Akipokea Rangi hizo RC Makalla amezigawa kwa Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji hilo kwaajili ya Kupaka kwenye Vyuma na Minyororo iliyowekwa pembezoni mwa Barabara za Jiji hilo.
Aidha RC Makalla ameishukuru kampuni ya Coral Paint kwa kushirikiana na Serikali kwenye mkakati wa kusafisha na Kupendezesha Mandahari ya Jiji la Dar es salaam.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Adam Kefa amesema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo Kupendezesha Mandahari ya Jiji Hilo ili kutimiza maono ya RC Makalla ya kuboresha Mandahari ya Jiji.